Wednesday, May 24, 2017

MAJINA YA WAHITIMU WA KIDATO CHA SITA WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA JKT 2017 HAYA HAPA






Wanafunzi wa kidato cha sita waliohitimu mwaka huu May 2017 takribani 14,747 sawa na asilimia 23.2%, wamepangiwa katika vituo mbalimbali vya Jeshi kati ya wahitimu 63,623, wanatakiwa kufika kambini kuanzia 25-30 May.

Taarifa imetolewa na Mkuu wa JKT

Akiongea na ITV amesema Orodha ya waliochaguliwa katika kambi mbalimbali yanapatikana katika tovuti yao ya JKT. www.jkt.go.tz

Source: ITV (Habari)





Ni hivi Majina yametoka na leo nilimsikia msemaji pale JKT akiongea kwenye Habari ITV, na idadi ya wanafunzi waliochaguliwa imepungua sana ndo maana leo Mbunge wa Newala akauliza Swali kwa Waziri wa Ulinzi ni kwanini Idadi hiyo imeshuka sana?


Pakua majina ya waliochaguliwa HAPA

=========

unnamed.jpg

TAARIFA KWA UMMA
Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), limechagua vijana waliohitimu Elimu ya Sekondari Kidato cha Sita kwa mwaka 2017, kutoka Shule zote za Tanzania Bara kuhudhuria mafunzo ya JKT kwa Mujibu wa Sheria.

Sanjari na Uchanguzi huo, JKT limewapangia Makambi watakayokwenda kupatiwa mafunzo kwa muda wa miezi mitatu na wanatakiwa kuripoti Makambini kuanzia tarehe 25 – 30 Mei 2017.

Vijana waliochanguliwa, wamepangiwa katika kambi za JKT Rwamkoma – Mara, JKT Msange – Tabora, JKT Ruvu – Pwani, JKT Makutopora – Dodoma, JKT Mafinga – Iringa, JKT Mlale – Ruvuma, JKT Mgambo na JKT Maramba – Tanga, JKT Makuyuni – Arusha, JKT Bulombora, JKT Kanembwa na JKT Mtabila – Kigoma.

Aidha, wahitimu wenye ulemavu wa kuonekana kwa macho (physical disabilities) wanatakiwa kuripoti kambi ya JKT Ruvu iliyopo Mlandizi mkoani Pwani ambayo ina miundombinu ya kuhudumia watu wa jamii hiyo.

JKT linawataka vijana hao kuripoti wakiwa na vifaa vifuatavyo:

JKT linawataka vijana hao kuripoti wakiwa na vifaa vifuatavyo:

1.Bukta ya rangi ya ‘Dark blue’ yenye mpira kiunoni (lastic), iliyo na mfuko mmoja nyuma, urefu unaoishia magotini, isiyo na zipu.


2.Raba za michezo zenye rangi ya kijani au blue.


3. Shuka mbili za kulalia zenye rangi ya blue bahari


4.Soksi ndefu za rangi nyeusi.


5.Nguo za kuzuia baridi kwa waliopangiwa mikoa yenye baridi.


6. Track suit ya rangi ya kijani au blue.


7.Nauli ya kwenda makambini na kurudi majumbani.


Mkuu wa JKT anawakaribisha Vijana wote waliochaguliwa ili waweze kujiunga na Vijana wenzao katika kujifunza Uzalendo, Umoja wa Kitaifa, Stadi za kazi, Stadi za maisha na Utayari wa kulijenga na kulitumikia Taifa letu.



Imetolewa na:


Kurugenzi ya Habari na Uhusiano,

Makao Makuu ya JKT,

Tarehe 22 Mei 2017


 Share  na  rafiki zako.



0 comments:

Post a Comment